Wito wa wafadhili

Fadhili CLEAR Global leo

Fursa yako ya kujiunga nasi katika mstari wa mbele katika utafiti wa lugha na teknolojia ya akili bandia (AI) kwa manufaa ya kijamii.

Je, una nia ya kutusaidia kupunguza mgawanyiko wa lugha ya kidijitali?

 

Leta athari za kweli za kijamii pamoja nasi.

CLEAR Global imezindua mkakati mkuu wa kukabili changamoto zinazozuia maendeleo ya kimataifa.  Tunatafuta wabia wa kimkakati ambao wanashiriki maono yetu ya usawa, na wanataka kuleta mageuzi mazuri duniani kote.

A group of people using Internet in a box, in Gubio northeast Nigeria, Nov 2019
Women working at desk

Je, uko katika sekta ya teknolojia, maudhui, mawasiliano au ujanibishaji?

Je, kampuni yako inaingiliana na maono yetu, na iko tayari kuchukua hatua?

Tunakualika ujiunge na harakati zetu – Mazungumzo Bilioni Nne.

– kwa sababu watu bilioni nne bado hawawezi kupata habari au kuwasiliana mtandaoni katika lugha yao.

Ikiwa kampuni yako imewekeza katika kukuza mazungumzo ya lugha nyingi, ushirikiano, maendeleo na uendelevu, jiunge nasi ili kuwezesha mtandao kufanya kazi kwa kila mtu, bila kujali lugha yake. 

Kwa usaidizi wa wafadhili wetu wakarimu, CLEAR Global imedhamiria kubadilisha jinsi ulimwengu unavyowasiliana. Timu yetu ya kimataifa ya wataalam hushirikiana na wazungumzaji na wanateknolojia wa lugha za ndani ili kujenga suluhisho za lugha za kibunifu, jumuishi na zinazofikika.

Tayari tumeunda robotisogoa za mazungumzo ya lugha nyingi, faharasa na nyenzo nyinginezoza mtandaoni ili kuwasaidia watu kupata habari muhimu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kaskazini mashariki mwa Nigeria, Ukreini, Uturuki na Syria, na zaidi.

Wafadhili wanaoweza kuchangia $25,000 au zaidi wanaweza kutusaidia kupanua shughuli zetu na kuongeza teknolojia ili kufikia jamii zaidi duniani kote.

Jifunze jinsi usaidizi wako unavyoweza kusaidia kubadilisha miundo ya mamlaka duniani na kujumuisha watu zaidi katika mazungumzo muhimu ya kimataifa, kuhusu uhamishaji wa kulazimishwaafya ya ummaafya ya uzazi na haki za wanawake, na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa nini uwe mfadhili wa CLEAR Global?

Kwa kuwa mfadhili wetu, utatusaidia kupanua programu zetu za usaidizi wa mawasiliano na suluhisho za teknolojia ya lugha, ili mamilioni ya watu wanaozungumza lugha zilizotengwa waweze kusikika na kupata habari muhimu, mara nyingi zinazoweza kubadilisha maisha yao. Utakuwa sehemu muhimu ya shirika letu.

Kama mfadhili wetu, kampuni yako itafaidika kutokana na kuongezeka kwa mwonekano, kuboreka kwa sifa ya kampuni, na kushirikiana na shirika lisilo la faida linalotetea utofauti na ujumuishi wa lugha na jamii. Viwango vyetu vyote vya ufadhili hutoa manufaa yafuatayo:

 • utambuzi wa chapa na kuthaminiwa ndani ya tasnia ya lugha, sekta ya msaada wa kibinadamu, na kwingineko,
 • uwekezaji unaotokana na madhumuni kama sehemu ya mkakati wako wa uwajibikaji kwa jamii,
 • athari ya moja kwa moja – kuboresha maisha ya mamilioni ya watu wanaozungumza lugha zilizotengwa,
 • nafasi ya kujiweka kama mtaalamu na kuchangia kuunda teknolojia ya hali ya juu ya lugha,
 • ufahamu katika lugha na data ya mawasiliano ambayo inaweza kukusaidia kurekebisha suluhisho zako, na kufikia watu wengi zaidi,
 • nafasi za kujitolea, mafunzo na maendeleo kwa wafanyakazi wako,
 • kuongezeka kwa mwonekano kupitia njia zetu za mawasiliano mtandaoni (tovuti, baruapepe, mitandao ya kijamii), na
 • athari za kimataifa kupitia ushiriki wa wafadhili katika mipango inayosaidia kubadilisha mazingira ya mawasiliano kuwa bora

Nani anafaa kuwa mfadhili wa CLEAR Global?

Ikiwa kampuni yako inaendeshwa kwa:

 • kufanya mtandao ufanye kazi kwa kila mtu, bila kujali lugha yao,
 • kukuza mawasiliano ya lugha nyingi kwa ushirikiano na maendeleo ya kimataifa,
 • kusaidia suluhisho za lugha za hali ya juu ya akili bandia (Al) ili kuboresha ufikiaji wa watu kwa habari, na
 • kuendeleza kazi ya timu za kimataifa, washirika wa ndani, na ushirikishi wa jamii
 

Wasiliana nasi ili kuona jinsi tunavyoweza kufanya kazi pamoja, na kujenga ulimwengu unaojumuisha zaidi lugha.

Saidia kazi ya CLEAR Global na huduma zako za bila malipo

Pia chaguzi zetu za ufadhili wa kifedha ili kusaidia TWB na CLEAR Global , na tunakukaribisha ujiunge na mpango wetu wa ufadhili usio wa kifedha. 

Ikiwa ungependa kusaidia kazi yetu na huduma za bila malipo, unaweza kuwazia kutoa::

 • Usaidizi wa kutafsirishirikiana nasi katika miradi ya utafsiri, masahihisho na ujanibishaji kulingana na uwezo wako na jozi za lugha unazopendelea
 • Msaada wa dharura: utusaidie kuitikia mahitaji ya dharura ya watu walioathiriwa na kuimarisha mwitikio wa kibinadamu katika dharura ikiwemo majanga ya kiasili, migogoro ya kisiasa au kijamii, afya ya umma na zaidi.)
 • Msaada wa kiteknolojia: kusaidia kupanua shughuli zetu na kuendeleza Ufumbuzi wa msingi wa akili bandia (AI) na programu za lugha na utafiti zinazotegemea teknolojia.
 • Usaidizi wa data na ufahamu: utusaidie kuchanganua na kuboresha data zetu ili tuweze kuboresha ufanisi na kuongeza ufikiaji wetu 

Mchango wako kama mfadhili wa bidhaa huongezeka athari tunayounda katika CLEAR Global kwa usaidizi wa jamii yetu ya Translators without Borders

Mpango wetu wa ndani unatambua ukarimu wa wale wanaotoa muda wao, teknolojia na utaalamu ili kutusaidia kufikia malengo yetu. Wafadhili wasio wa kifedha hufaidika kwa mwonekano ndani ya jamii kubwa zaidi msaada wa kibinadamu duniani na maendeleo – wanalugha wanaojitolea. Pata habari zaidi kuhusu TWB – jamii yetu ya kimataifa ya zaidi ya watu 100,000.

Wafadhili wetu

Wafadhili wetu wanajumuisha kampuni na mashirika kutoka sekta mbalimbali. Wote wanakuja pamoja kuchangia maono yetu ya pamoja, kusaidia watu kupata habari muhimu na kusikilizwa, kwa lugha yoyote wanayozungumza. Tungependa kushukuru:

Pia tunathamini usaidizi wa wafadhili wetu wa Jamii ya TWB. Pata habari zaidi kuwahusu kwenye tovuti ya TWB.

Kampuni yangu inaweza kusaidia kwa njia nyingine zipi?

Ikiwa ungependa kusaidia kazi yetu, unaweza kutoa mchango mkubwa zaidi. Mchango wako utasaidia kufadhili miradi mahususi, ambayo tunaweza kuzingatia pamoja. Usaidizi wa aina hii una thamani sawa na unathaminiwa – miradi kwa kawaida huhitaji fedha kati ya $25,000 na $100,000.