CLEAR Global logo

Zungumza kwa ajili ya

Ujumuishaji wa Lugha

Lugha ndio ufunguo

Kukidhi Malengo ya Maendeleo Endelevu:

Jinsi ya kutomwacha mtu yeyote nyuma – katika lugha yoyote wanayozungumza 

Rasilimali zilizojanibishwa zinasaidia kuunda hatua jumuishi na endelevu ya hali ya hewakwa wale walioathiriwa zaidi.

Suluhu za habari jumuishi za afya, utafiti na teknolojia bunifu zinaweza kusaidia kufikia afya kwa wote.

Kuwasaidia watu kupata habari muhimu, na kusikilizwa, katika lugha yoyote wanayozungumza.

Tunatimiza dhamira hii kupitia utafiti na programu bunifu za kimataifa, teknolojia ya lugha, majukwaa ya huduma za lugha, wafanyakazi wenye uzoefu na taaluma, na jamii ya zaidi ya wanaisimu 100,000 katika nchi 148.

Iwe ni robotisogoa ya COVID-19 nchini Nigeria, mafunzo ya watafsiri nchini Kenya au utafiti wa lugha katika kambi za wakimbizi wa Rohingya, kazi yetu inasaidia mashirika kuwasiliana kwa ufanisi zaidi, ili yaweze kufikia watu zaidi, kusikiliza kwa makini na kuboresha matokeo.

Asilimia 28

Asilimia 28 ya wakimbizi wa Rohingya waliohojiwa mwaka wa 2018 walisema hawana taarifa za kutosha ili kufanya maamuzi sahihi.

Bilioni 4

Kuna takriban watu bilioni 4 wanaozungumza lugha iliyotengwa, jambo ambalo linawaacha nje ya mazungumzo muhimu ya kimataifa.

Zaidi ya 80

Tumeunga mkono programu na mashirika yaliyopo katika nchi Zaidi ya 80 na katika lugha Zaidi ya 220.

Njia mpya za kuwawezesha watu kupitia lugha na teknolojia

Translators without Borders

Uwezo wa wanaisimu zaidi ya 100,000 wanaojitolea waliojitolea kuziba mapengo ya lugha ya ulimwengu na kuitikia kwa umakini zaidi katika mahitaji.

Idara ya Teknolojia ya CLEAR

Tunaanzisha teknolojia ya ubunifu ili kushirikiana na watu wengi kwa njia zinazowafaa zaidi.

Idara ya Utafiti ya CLEAR

Tunatafuta njia mpya za kusikiliza watu na kufanya utafiti ili kutetea ujumuishaji wa lugha na teknolojia katika kazi ya utoaji misaada.

Jamii kubwa zaidi duniani ya wanaisimu wa kibinadamu, Translators without Borders

Jamii yetu ya kimataifa ya wanaisimu na watafsiri zaidi ya 100,000 ni msingi wa dhamira yetu. Shauku na utaalamu wao unaziba mapengo ya lugha duniani kote.

Jukwaa la TWB

Jukwaa letu huunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali na wanaisimu ili kutoa habari za afya, miitikio ya kibinadamu, na taarifa za haki za binadamu zipatikane katika lugha za wenyeji.

Huduma za lugha

Huduma zetu za lugha zinasaidia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya kimataifa na ya eneo kushirikiana kwa ufanisi zaidi na watu wanaoishi katika mizozo. Tunasaidia kutoa habari muhimu kwa haraka, katika lugha inayofaa.

Suluhisho za teknolojia na data

Kwa kuwafunza watafsiri na wafasiri, kuunda faharasa za lugha nyingi, na kushirikiana katika utafiti na teknolojia, tunaimarisha uwezo wa lugha.

Tembelea tovuti ya Translators without Borders.

"Sikuwahi kufikiria kuwa lugha yangu inaweza kuzingatiwa kuwa muhimu sana hivi kwamba iweze kuwekwa kwenye kifaa.”

Mawasiliano ya pande mbili ni muhimu. Teknolojia inasaidia kuyaboresha. Kutana na Idara ya Teknolojia ya CLEAR.

Tunageuza teknolojia yetu ya lugha kuwa bidhaa na huduma zinazolingana na miktadha ya eneo husika, na ambazo watu na washirika wanaweza kutumia kwa urahisi zaidi.

Mawazo yanayoweza kuboresha

Tunatumia teknolojia za sauti, Akili Unde, na tafsiri kutumia mashine ili kupanua kwa kiasi kikubwa idadi na ubora wa mazungumzo ambayo yanayoendesha mabadiliko.

Majukwaa yanayosaidia

Teknolojia yetu imejengwa kuwa wazi, hivyo wavumbuzi wengine wanaweza kuijumuisha katika kazi zao wenyewe. Hii inazidisha ufikiaji na matokeo.

Kufikia zaidi, kusikiliza kwa makini zaidi

Tunaanzisha njia mpya za kushirikiana na watu kila mahali—hata katika maeneo yenye muunganisho hafifu na elimu ya chini.

Jifunze jinsi unavyoweza kuhusika na Idara ya Teknolojia ya CLEAR.

Njia mpya za kusikiliza, kuwajibika, na kutetea uwezo wa mazungumzo. Kutana na Idara ya Utafiti ya CLEAR.

Lugha inaweza kuzuia kazi ya misaada. Hii ndiyo sababu ya sisi kusikiliza kwanza— kufanya utafiti wa kibunifu ili kuelewa mapendeleo ya mawasiliano ya watu na ni habari gani hasa wanayotaka na kuhitaji. Tunatumia data hii kuvumbua njia mpya za kusikiliza—na kuuonyesha ulimwengu nguvu ya ushiriki wa kijamii unaowajibika.

Data ya lugha shirikishi na ramani

Inasaidia wahudumu wa misaada ya kibinadamu kujua mapendeleo ya lugha na mawasiliano ya wenyeji, ili waweze kuwasiliana kwa ufanisi zaidi na kuhusisha watu vilivyo.

Mifano ya visa

Kutetea lugha na 'msaada unaosikiliza kwanza'—kipengele muhimu cha msaada wa kimataifa.

Miongozo na habari

Inaeneza mazoea bora zaidi kuhusu lugha zenye ufanisi zaidi, miundo, na njia ili kukuwepo na mawasiliano yenye ufanisi.

Idara ya Utafiti ya CLEAR inasikiliza kwanza. Jihusishe.

Unaweza kusaidia.

Mtindo huu unafanya kazi. Hitaji ni kubwa—watu wengi wanaachwa nyuma kila siku, kwa sababu tu ya lugha wanazozungumza. Mtazamo huu umethibitishwa—tena na tena. Lakini tunahitaji fedha ili kuimarisha.

Tumekua zaidi ya jina letu.

CLEAR Global ilikuwa ikiitwa Translators without Borders. Tumekua kwa kasi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na jina hilo halijumuishi yote tunayoyafanya—lakini bado lipo kama kitengo chetu kikubwa zaidi na kiini cha kazi yetu. Tembelea tovuti ya TWB hapa.