CLEAR Global logo

mazungumzo bilioni 4

Mtandao umeleta mapinduzi makubwa katika mawasiliano. Yametupa ufikiaji usio na kikomo wa habari, na kuturuhusu kuungana kama kamwe hapo awali, popote tulipo. Hata hivyo, nyenzo za lugha, kama vile tafsiri ya mashine, utambuzi wa usemi kiotomatiki, na akili bandia (AI) ya mazungumzo, pamoja na manufaa makubwa wanayoleta (ujumbe wa papo hapo, mawasiliano ya njia mbili, data wazi), zinapatikana tu kwa nusu ya idadi ya watu duniani. Watu bilioni nne hawawezi kuunganishwa na kupata habari katika lugha yao.
A hand of an African person holding a mobile phone

Zaidi ya watu bilioni 4 kwenye sayari hawawezi kupata habari au kuwasiliana kwa njia ya kidijitali, kwa sababu ni kidogo au hakuna chochote kinachopatikana katika lugha wanazozungumza.

Ni wakati wa kuchukua hatua.

Ingawa kuna mlipuko wa talanta katika teknolojia ya lugha kote Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia Kusini, na kwingineko, jamii hizi za teknolojia hazina nyenzo za kuongeza kasi. Na matumizi ya teknolojia hii ibuka ya lugha kwa lugha zilizotengwa yanaendelea polepole. Pengo la lugha ya kidijitali linaongezeka.

Ni wakati wa kuchukua hatua, na hatuwezi kufanya hivi peke yetu. Tunahitaji msaada wako. Tuna fursa ya kutumia teknolojia kuendesha maendeleo, kuunda usawa zaidi, na kuwapa watu uwakala katika maisha yao wenyewe.

CLEAR Global inaunganisha utaalamu wake katika kutumia akili bandia (AI) ya lugha kwa kiwango na miongo kadhaa ya uzoefu wa kimataifa wa usaidizi kushughulikia mgawanyiko wa lugha ya kidijitali. Mchanganyiko huu wa kipekee wa ujuzi utaturuhusu kufanya kazi kama kichocheo cha mabadiliko, kujenga masuluhisho ya lugha yanayoendeshwa na akili bandia (AI) na athari ya juu ya kijamii.

Unaweza kusaidia.

Tunaomba msaada wako. Tunatafuta washirika wa mpango wa athari za kijamii, wanateknolojia wa ndani, mipango ya msingi, wafadhili, wahisani, na wengine ili kusaidia kuleta watu bilioni 4 wanaofuata kwenye mazungumzo ya kimataifa, na kuanzisha yao, ya ndani. Utajiunga nasi?

Fikia watu wengi zaidi

Changia kusaidia bilioni 4 zijazo

Jifunze zaidi

Wasiliana ili kushirikiana au kufadhili harakati.