Kazi
Kuwa sehemu ya mabadiliko. Fanya kazi yako iwe muhimu. Jiunge na CLEAR Global.
CLEAR Global huwasaidia watu kupata habari muhimu na kusikilizwa, kwa lugha wanayozungumza. Timu yetu ya kimataifa inajikaza kufikia lengo hili.
Kuwa sehemu ya mabadiliko. Fanya kazi yako iwe muhimu. Jiunge na CLEAR Global.
CLEAR Global huwasaidia watu kupata habari muhimu na kusikilizwa, kwa lugha wanayozungumza. Timu yetu ya kimataifa inajikaza kufikia lengo hili.
CLEAR Global inaendeleza mazoea kwa msingi wa mawasiliano ya wazi, heshima, na uaminifu. Ikiwa utajiunga nasi, utakuwa sehemu ya timu ya watu tofauti kutoka ulimwenguni kote.
Ukiwa nasi, utashirikiana na kuwa mbunifu kwa timu. Mchango na maoni yako daima yatathaminiwa, kuzingatiwa, na kujumuishwa mara kwa mara.
Kikundi chetu cha Utofauti, Usawa, na Ujumuishaji hufanya kazi kwa pamoja na uongozi wetu kufanya CLEAR Global kuwa shirika ambapo kila mtu anaheshimiwa na kutendewa kwa heshima. Aina yoyote ya ubaguzi au unyanyasaji kamwe haitaruhusiwa katika CLEAR Global. Tunachukulia kazi yetu kwa umakini, na tunawajibika kwa kila mmoja. Kile tunachofanya kinaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu wengine. Tunataka kufanya uzoefu wako kuwa wa kuridhisha.
Ikiwa ungependa kujiunga na timu ya kimataifa inayojikaza kubadilisha mazingira ya mawasiliano ya kimataifa, tazama fursa zetu za kazi na utumi maombi hapa chini:
Mazoea yetu yamejikita katika maadili sita ya msingi tunayoendeleza kama shirika lisilo la faida kwa madhumuni muhimu:
Kama sauti inayoongoza kwa kuwasilisha habari za msaada wa kibinadamu kwa lugha sahihi, CLEAR Global ni kiongozi katika sekta ya tafsiri na katika sekta isiyo ya faida.
CLEAR Global inaamini kwamba kila mtu, iwe ni watu tunaowahudumia, wanalugha wetu au wafanyakazi wetu, ana thamani, anastahili heshima, na ana heshima ya asili.
CLEAR Global inaamini katika kutumia lugha kuwawezesha watu duniani kote kudhibiti maendeleo yao wenyewe na hatima yao.
CLEAR Global inatambua na kusherehekea nguvu ya ubunifu kushughulikia masuala ya kibinadamu na migogoro duniani kote.
CLEAR Global inatambua kwamba kufikia lengo letu kunahitaji uanzishaji na udumishaji wa miundombinu imara ya kifedha na shirika.
Wafanyakazi na wanalugha wetu wana ufahamu na ujuzi wa juu; kuthamini kila mmoja, washirika wetu na wapokeaji huduma zetu; kujenga mazingira ya kazi ya kusaidia; na kujiendesha kwa weledi wakati wote.
Raia wa Marekani na waombaji kazi walio nchini Marekani wanapaswa kutambua kwamba tunashiriki katika E-Verify, na kwamba tunaheshimu haki ya kila mtu ya kufanya kazi. Hatubagui kwa misingi ya uraia, hadhi ya uhamiaji au msingi mwingine wowote. Ikiwa una idhini ya kisheria ya kufanya kazi, kuwa na ujuzi, kuendesha gari, na uzoefu, tungependa kusikia kutoka kwako!
CLEAR Global inafanya kazi hasa kwa mbali – hii inatupa kubadilika tunakohitaji kufanya kazi na kutofautisha timu zetu. Inatusaidia kupunguza gharama za juu, kwa hivyo tunaweza kuwekeza fedha zaidi katika kusaidia watu. Mwisho, inatusaidia kupunguza athari zetu kwa mazingira.
Tunapofanya kazi katika mazingira ya haraka, tunakuza mahali pa kazi wazi ili kuhimiza ubunifu, tija, na ushiriki. Tunafanya kazi kwa bidii ili kudumisha mazoea ya kirafiki na wazi. Timu yako itatia bidii kuhakikisha unaelewa kazi yetu na jukumu lako kutoka siku ya kwanza.
Tunategemea zana za mtandaoni kuwasiliana na kuungana. Tuna mikutano ya kila mwezi ya timu zote, ambapo tunashiriki habari na sasisho, kucheka, na kujuana vizuri. Pia tunaandaa mawasilisho ya timu, warsha, na vikao vingine ambavyo vinatusaidia kujifunza na kufanya kazi vizuri.
Tunajitahidi kuwafanya watu wetu wajisikie kuthaminiwa na kutambuliwa. Mbali na malipo bora, tunatoa pia:
Kama mfanyakazi wa kijamii anayeongoza kwa shirika lisilo la kiserikali, nilitumwa kwa jamii, pamoja na timu yangu. Ni mimi tu niliyeelewa lugha ya wenyeji. Ilikuwa vigumu sana kwetu kupata wakalimani. Tulijaribu kuwasiliana na watu. Muda mfupi baadaye, niligundua CLEAR Global na jitihada zao za kuondoa vizuizi vya kilugha kaskazini mashariki mwa Nigeria. Nilijiwekea lengo la kukuza sauti za watu wasiosikika na hivyo kujiunga na CLEAR Global.
Kufanya kazi katika CLEAR Global ni uzoefu wenye kutajirisha kweli. Mimi hupata kutumia hamasa yangu ya lugha kila siku kutetea mambo muhimu, na kushughulikia mojawapo ya changamoto kubwa katika sekta ya kibinadamu. Siyo tu kwamba nafanya kazi pamoja na kundi la wenzangu wenye nia moja, wenye vipaji na washirika, lakini pia nimepata usawa wa thamani wa maisha ya kazi.
Siku zote mimi huhisi kuwa hii ni zaidi ya kazi kwa sababu akili yangu huwa ikinikumbusha kwamba kila kipengele cha kazi yangu kinahusu kuwasaidia watu kutoka duniani kote kuondoa vizuizi vya kilugha. Kwa kweli, ni motisha kubwa ya kuendeleza kazi!
Nafurahia kufanya kazi katika CLEAR Global, kwa sababu ni mazingira ya kazi ya kirafiki na ya haraka ambapo unaweza kujifunza na kuendelezwa kama mtaalamu wakati unafanya kazi kwenye miradi ya kibinadamu ili kupata habari muhimu kwa wale wanaohitaji. Ni jambo la kufurahisha sana kujua kwamba juhudi zetu zote zinaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu wanaohangaika kupata habari, hasa wakati wa shida. Ningekuhimiza ujiunge na CLEAR Global ikiwa ungependa kuhusika katika shirika linaloleta mabadiliko ambalo linaleta athari kubwa katika jumuiya tofauti.
CLEAR Global inanipa fursa ya kusaidia jamii yangu kupata habari za kuokoa maisha katika lugha yangu mwenyewe na kusikika ingawa lugha yangu inachukuliwa kama iliyotengwa kaskazini mashariki mwa Nigeria. CLEAR Global pia inanipa ufahamu na kufungua macho yangu kwa umuhimu wa lugha kama muhimu katika kila kazi ya kibinadamu. CLEAR Global inajali lugha zilizotengwa, na daima iko tayari kusaidia. Kwa sababu hii, ninaiona kuwa moja ya shirika lisilo la kiserikali bora zaidi ambazo nimewahi kuzijua na kufanya kazi nazo hadi sasa. Habari ni nguvu na habari ni maisha - mtu anayetoa habari sahihi anaokoa maisha ya watu - kama vile CLEAR Global inavyofanya.
Kuomba kazi kunahitaji muda na juhudi. Tunajaribu kuwa wazi iwezekanavyo wakati wote wa mchakato wa kuajiri.
Bonyeza ili ujifunze zaidi kuhusu kila hatua ya mchakato.
Nambari ya Hisani iliyosajiliwa Ireland: 20073459