Mazungumzo ya bilioni nne kuhusu
Hapa CLEAR Global, tunawapa mabinti na watoto wa kike nafasi ya siri na salama ili kuuliza maswali, kushiriki wasiwasi, na kutafuta msaada, katika lugha yoyote wanayozungumza.
Tatizo: wanawake wanahitaji kujifunza na kuzungumza kwa uwazi kuhusu afya yao
- Wanawake duniani kote wanakumbana na shutuma, inayowazuia kuzungumza kwa uwazi na kupata taarifa kuhusu afya yao ya uzazi na haki.
- Ukosefu wa kupata taarifa na elimu kunawaweka wanawake, hususan watoto wa kike na mabinti, katika maambukizi mbalimbali kwa njia ya ngono (STI). STI huathiri ustawi wa wanawake kupitia shutuma, ugumba, na hata saratani na matatizo ya mimba.
- Zaidi ya asilimia 95 ya vifo vya uzazi hutokea katika nchi zinazoendelea, kukiwa na ukosefu wa taarifa ya afya na huduma bora ikiwa ni sababu kubwa.
“Mawasiliano mazuri ni muhimu iwapo tunataka watu waliotuhumiwa ambao tayari wameumizwa sana wapate msaada sahihi. Robo tatu ya wanawake wa Rohingya katika makambi walisema hawakujisikia salama kuacha makazi yao - tunahitaji kuelewa kwa kina kwa nini jambo hili liko hivi, ili tuweze kufanya kazi nzuri kuwalinda wanawake.”
Suluhisho ya CLEAR Global
CLEAR Global hushirikiana na mashirika ya haki na afya ya wanawake ili kufanya taarifa kuhusu ngono na afya ya uzazi inapatikana katika lugha na miundo ambayo wanawake wanaelewa. Kwa kutumia tatuzi zetu bunifu za mawasiliano, wanawake wanaweza kupata rasilimali za elimu, huduma ya afya na msaada. Pia, wanaweza kushiriki wasiwasi wao na kupokea majibu kwa usalama na uhakika.
Wakati wa ukabilianaji wa virusi vya Zika, tulifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kuzalisha video muhimu zenye ushauri kwa wanawake wajawazito na kuwekwa maelezo na sauti katika Krioli ya Haiti na Kireno cha Brazili nchini Haiti na Brazili.
Nchini Kenya, tafsiri zetu za nyenzo za elimu na huduma ya vipeperushi vya huduma ya afya kwa kliniki za jamii zilisaidia wafanyakazi wa afya wa kijijini na watoa elimu kufikisha taarifa kuhusu dondoo za unyonyeshaji wa mtoto mchanga katika lugha za ndani kwa mara ya kwanza.
Tuliongoza makundi ili kuelewa vema jinsi wanawake wa Rohingya nchini Bangladesh wanavyozungumza kuhusu afya yao na tuhuma. Tuliunda rasilimali za lugha, kama vile faili za sauti na faharasa, kwa kuwasaidia wafanyakazi kutatua vema mahitaji ya wanawake.
CLEAR Global inahitaji msaada wako katika
kuwapa wanawake njia nyingi zaidi za kujifunza kuhusu afya yao ya uzazi na haki.
kuwapa wanawake njia nyingi zaidi za kujifunza kuhusu afya yao ya uzazi na haki.