CLEAR Global, hapo zamani ilijulikana kama Translators without Borders, ni shirika lisilo la faida la Marekani linalosaidia watu kupata habari muhimu na kusikika, katika lugha yoyote wanayozungumza. Kwa kutumia suluhisho bunifu za teknolojia ya lugha, tafiti, na jamii ya wanaisimu zaidi ya 80,000, CLEAR Global husaidia mashirika washirika yanayofanya kazi katika mazingira mbalimbali duniani kote.

 

Shirikiana nasi

Huduma zetu za lugha na mawasiliano zinaweza kukusaidia kuwafikia watu wengi zaidi.

Tunajenga mahusiano ya muda mrefu pamoja na mashirika yasiyo ya faida na mashirika yasiyo ya kiserikali. Tunatoa huduma mbalimbali za lugha na mawasiliano ili kuongeza matokeo na kukusaidia kuwafikia mamilioni ya watu wanaozungumza lugha iliyotengwa au walioathiriwa na janga.

 

Students in the classroom

 

Huduma za CLEAR Global zinajumuisha tafsiri na uhariri, huduma za picha za video, tafsiri ya tovuti kwa muktadha, uundaji wa faharasa, pamoja na teknolojia ya lugha ya Akili Bandia (AI), data za lugha, na suluhisho za utafiti kwa msaada wa kibinadamu wenye ufanisi zaidi na endelevu.

 

Tunaweza kusaidia mashirika ambayo:

Fanya programu yako kuwa jumuishi zaidi. 

Wafikie watu wengi zaidi – katika lugha yao.

Baadhi ya washirika wetu

Jaza fomu hii ili uanze.