Mwitikio wa wakimbizi

Kuwasaidia watu walio lazimika kuyahama makaazi yao

Kila mtu ana haki ya kupata habari muhimu na kusikilizwa, haijalishi anazungumza lugha gani

Rohingya refugee camp in Bangladesh

Ulimwenguni kote, idadi ya watu waliolazimika kuyahama makaazi yao imefikia rekodi ya milioni 100.

Zaidi ya theluthi mbili ya wakimbizi wanatoka nchi tano tu: Syria, Venezuela, Afghanistan, Sudan Kusini, na Myanmar.

Mzozo wa Ukraine umewalazimu zaidi ya watu milioni sita kukimbia.

Popote wanapotoka, watu walio yahama makaazi yao wanahitaji msaada – kuzoea maisha mapya, kupata makazi, kazi, elimu.

Lakini, wote wanakabiliwa na vikwazo vya lugha na mawasiliano.

CLEAR Global inafanya kazi kukabiliana na vizuizi hivi. Tunasaidia wakimbizi kupata habari muhimu wanazohitaji ili kuunganishwa kwa usalama katika nchi mpya. Tunatoa suluhisho za lugha ambazo husaidia watu kupata majibu ya maswali yao katika lugha wanayoelewa. Utaalam wetu husaidia kuziba mapengo ya mawasiliano kati ya wakimbizi na jumii zinazowapokea – haijalishi wanazungumza lugha gani.

Rohingya woman during a focus group session

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ambavyo tumeunga mkono huduma za wakimbizi huko Ulaya, Asia Kusini, na Amerika Kusini.

Mwitikio wetu wa wakimbizi wa Ukraine

Zaidi ya watu milioni 6 wamekimbia Ukraine, wakihamia Poland, Hungaria, Slovakia, Romania, Moldova, na nchi nyinginezo. Mara moja tulipanga timu ya kutoa usaidizi wa lugha bila malipo kwa nchi zinazowapokea na mashirika yanayotoa huduma. Pia tulituma wafanyakazi wetu wa kimataifa kwa nchi tano mwenyeji ili kutathmini mahitaji na njia za lugha na mawasiliano. Tumeunda nyenzo nyingi za lugha na nyenzo za mafunzo kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na madhumuni ya kibinadamu. Kufikia sasa, tumetafsiri zaidi ya maneno milioni 1.3 kama sehemu ya miradi 178 iliyokamilishwa kwa ushirikiano na mashirika 31. Pata maelezo zaidi kuhusu mwitikio wa CLEAR Global kwa wakimbizi wa Ukraine.

Ukrainian refugees in Poland
Rohingya child refugees in Bangladesh

Mwitikio wetu wa wakimbizi wa Rohingya

Zaidi ya watu 600,000 wa Rohingya walikimbilia Bangladesh mwaka wa 2017. Lugha ya Rohingya ni mojawapo ya lugha zilizotengwa zaidi duniani. Pamoja na uwezo mdogo wa kutafsiri, mawasiliano kati ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na watu wa Rohingya yalikuwa – na ni – magumu sana. Tulituma timu hadi Cox’s Bazar, Bangladesh, ili kujenga uwezo wa lugha na rasilimali ili kuwezesha mawasiliano na kusaidia kuboresha mwitikio wa kibinadamu.

Leo, kuna karibu watu 900,000 wa Rohingya katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh. Bado wanapitia magumu na wanahitaji msaada. Tuna ofisi za kudumu na timu iliyojitolea ya Bangladesh inayofanya kazi bila kuchoka kusaidia watu wa Rohingya kupata habari wanazohitaji na kuelewa. Tumeunda rasilimali nyingi juu ya utamaduni wa Rohingya, mahitaji ya habari na mawasiliano na mapendekezo, na kukamilisha miradi 49. Tutaendelea kufanya zaidi.

Faharasa na karatasi ya ukweli za lugha ya Rohingya 

Faharasa zetu za lugha ya Rohingya kwa Myanmar na Bangladesh kusaidia mawasiliano kati ya wafanyakazi wa misaada na jamii ya Rohingya kwa tafsiri zilizo wazi na sahihi za istilahi muhimu. Karatasi ya ukweli ya lugha ya Rohingya inakamilisha uelewa wa lugha.

Mapendeleo na mitazamo ya maelezo ya Rohingya

Moja ya ripoti zetu za hivi karibuni husaidia kuelewa mapendeleo ya Warohingya Inapohusu kwa lugha na miundo ambamo wanapokea habari. Pamoja na lugha nyingine inahitaji rasilimali, utafiti huu hurahisisha mawasiliano na uelewa wa kitamaduni.

Njia za malalamiko na maoni: wanawake na watu wenye uhamaji uliozuiliwa

Katika mwitikio wa wakimbizi, tunasaidia kuhakikisha mawasiliano ya njia mbili, na kwamba sauti za watu zinasikika, yeyote yule. Tuliwahoji wakazi wa kambi ya Rohingya kuhusu kushiriki maoni na kutoa malalamiko. Matokeo na vidokezo vyetu vinapatikana ndani ya ripoti hii.

Mwitikio wa wakimbizi wa Ulaya

Tulizindua mpango wetu wa mwitikio wa Maneno ya Usaidizi mnamo Septemba 2015. Ulilenga kusaidia mashirika ya misaada ya kibinadamu ya ndani na ya kimataifa kusaidia wakimbizi na wahamiaji wanaowasili kwa kiasi kikubwa kutoka Syria, Afghanistan, na Pakistan. Tulitafsiri takriban maneno 800,000 ya maudhui ya umbizo nyingi katika Kiarabu, Kiajemi, Kigiriki, Kikurdi na Kiurdu. Mashirika yetu washirika yanakadiria kuwa tumesaidia takriban watu 100,000 kupata habari kuhusu ulinzi, taratibu za kupata hifadhi na huduma za kimsingi katika lugha yao.

Pia tulipanga vipindi vya mafunzo ya moja kwa moja kwa wakalimani, na kuunda faharasa za lugha, karatasi za ukweli, na ripoti za tathmini ya mawasiliano kwa wanaokabiliana ili kuwasiliana nao vyema, kusikiliza na kushughulikia mahitaji ya wakimbizi. Unaweza kupata baadhi ya rasilimali hapa chini.

European refugee response - Greece

Vikwazo vya lugha na ufahamu katika mgogoro wa kibinadamu wa Ugiriki – muhtasari wa kiutendaji

Huu ni muhtasari mkuu wa utafiti uliofanywa Aprili 2017 na TWB na Save the Children kuhusu vizuizi vya lugha na mawasiliano katika muktadha wa janga la kibinadamu linaloendelea Ugiriki.

TWB huduma za lugha katika mwitikio wa wakimbizi wa Ulaya

Jifunze kuhusu huduma tunazotoa kupitia mpango wetu wa Maneno ya Usaidizi kama sehemu ya mwitikio wetu wa 2015 kwa wakimbizi nchini Ugiriki. Pia tulitoa rasilimali bila malipo kwa washirika wetu na watu wengine wanaowahudumia.

Faharasa za lugha na taarifa za ukweli

Karatasi zetu za ukweli katika KiarabuKikurdiKifarsi na Kidari, pamoja na faharasa yetu kuhusu mwitikio kwa wakimbizi nchini Ugiriki, huwasaidia watendaji kujifunza kuhusu lugha zinazozungumzwa na wakimbizi, ili kuboresha mawasiliano na mwitikio kwa wakimbizi.

Chatbot Planeta Azul OIM

Mwitikio wetu wa wakimbizi wa Amerika ya Kusini

Kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, tulitengeneza robotisogoa ya lugha ya Kihispania kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi wa Venezuela nchini Peru na Ecuador, pamoja na wakimbizi wa Amerika ya Kati na wanaotafuta hifadhi nchini Mexico.

Kama programu ya kompyuta inayoiga mazungumzo ya binadamu kwenye programu na vifaa, Planeta Azul Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (OIM) ilitoa habari muhimu kuhusu huduma za Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), na mada nyinginezo za kuvutia kwa jumuiya zilizoathiriwa. Robotisogoa ilijibu maswali ya watu kwa wakati halisi, na kuunda hali ya mazungumzo inayopatikana kupitia maandishi na video. Kwa njia hii, watu wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na robotisogoa katika lugha yao wenyewe, na kupokea habari wanayohitaji na kuelewa – bila kujali viwango vyao vya kusoma na kuandika au maneno yaliyotumiwa.

Watu wanaokimbia nchi zao wanahitaji na wanastahili kupata habari muhimu na kusikilizwa, lugha yoyote wanayozungumza, popote wanapotoka. Ndiyo maana mipango mipango yetu ya kuwahudumia wakimbizi inaendelea na inabadilika. Kwa kutumia data ya lugha, huduma na teknolojia, tunaweza kufikia na kuwasaidia watu wengi zaidi. Tafadhali unga mkono kazi yetu.