Mazungumzo ya bilioni nne kuhusu

mabadiliko ya tabianchi

Hapa CLEAR Global, tunasaidia watu katika dharura za tabianchi wapate taarifa ya kuokoa maisha, haijalishi wanazungumza lugha gani.

Tatizo: watu wanahitaji taarifa ili kujilinda dhidi ya majanga ya tabianchi

  • Majanga ya mabadiliko ya tabianchi yaliongezeka kwa asilimia 83 kwa miaka 50 iliyopita, yakisababisha uharibufu mkubwa.
  • Hali ya hewa mbaya huathiri kilimo, uchumi, na ustawi wa watu. Makundi yaliyo hatarini, kama vile watu wenye afya dhaifu au wenye rasilimali chache, huathirika haswa. 
  • Kukosekana kwa usalama wa chakula kumeongezeka katika miaka sita iliyopita, kukiathiri asilimia 30 ya idadi ya watu duniani. Mavuno ya mazao yanaweza kupungua kwa hadi asilimia 30 ifikapo 2050, na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

“Kimbunga Haiyan kilipokaribia Ufilipino, Translators without Borders walijibu ombi letu kwa haraka, kusaidia kufuatilia mitandao ya kijamii katika lugha na ujumbe wa maandishi na video uliotafsiriwa. Msaada huo ulisaidia kuokoa maisha na pia ulitoa ujumbe kufikisha msaada ili kuziunganisha familia ambazo zilikuwa zimeokolewa."

Chris Thompson
Humanity Road

Suluhisho ya CLEAR Global

Kwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya tabianchi katika miundo na lugha nyingi, CLEAR Global husaidia watu kuelewa mabadiliko ya tabianchi na hatua wanazoweza kuchukua ili kujiandaa na kujilinda.

Nyenzo zetu za data za lugha na mawasiliano hutumika katika dharura ili kuboresha mawasiliano ya pande mbili kati ya watoa msaada wa kibinadamu na watu walioathiriwa na majanga ya mabadiliko ya tabianchi. Hii husaidia hatua yenye ufanisi katika janga, hususan katika jamii zenye lugha nyingi ambazo mara nyingi huathiriwa zaidi na mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa.

Huko Nchi za Amerika, tuliweka timu za haraka za ukabilianaji katika hali mbalimbali za majanga ya kimbunga. Zaidi ya watu 100 alitafsiri maneno 15,000 ya mwongozo muhimu kuhusu usimamizi wa malazi, kujiandaa dhidi ya dhoruba, na tulizo katika lugha sita.

Huko Nepal, timu yetu ilifanya kazi 24/7 pamoja na mashirika ya msaada wa kabilianaji wa kwanza ili kutafsiri ujumbe kutoka kwa watu walioathiriwa na tetemeko, mitandao ya jamii ya wastani, kutafsiri hati za huduma ya kwanza, na kutafsiri video kwa maandishi ili kuboresha ukabilianaji.

Nchini Msumbiji, baada ya Kimbunga Idai, tulitoa msaada wa lugha, ikijumuisha tafsiri, data za lugha, na ramani. Tulitoa taarifa muhimu taarifa muhimu katika lugha mbalimbali ili kusaidia watu kujifunza jinsi ya kujilinda, kupata malazi, kuomba msaada wa ziada, na zaidi.

CLEAR Global inahitaji msaada wako katika

kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi