Mazungumzo ya bilioni nne kuhusu

uhamisho wa kulazimishwa

Hapa CLEAR Global, tunasaidia wakimbizi na wahamiaji kupata taarifa muhimu na kusikilizwa, haijalishi wanazungumza lugha gani.

Tatizo: vizuizi vya lugha huathiri ushirikiano wa kijamii na kiuchumi

  • Kufikia 2022, zaidi ya watu milioni 100 walilazimika kukimbia nchi zao kwa sababu ya migogoro, uhaba wa chakula, hali ya hewa au dharura zingine.
  • Vizuizi vya lugha huleta ugumu kwa wakimbizi na wahamiaji kupata kazi, elimu, usaidizi muhimu na huduma, kama vile afya na makazi.
  • Nchi mwenyeji na mashirika ya misaada mara nyingi hukosa uwezo wa lugha na rasilimali ili kuelewa vyema na kusaidia watu wanaotafuta hifadhi.

"Tulifanya maajabu hapa... taratibu za kisiwa hatimaye ziko katika muundo unaoweza kufikiwa na kila mtu."

Refucomm
Mshirika nchini Ugiriki/Maneno ya Usaidizi

Suluhisho ya CLEAR Global

CLEAR Global hufanya utafiti kuhusu lugha za watu, mahitaji ya taarifa na mapendeleo. Maarifa yetu husaidia kuunda njia za mawasiliano ambazo watu wanaweza kutumia kupata taarifa wanazoamini na kuelewa. Kwa njia hii, watu waliolazimika kuyahama makaazi yao wanaweza kufikia rasilimali za kuokoa maisha zilizochukuliwa kulingana na mahitaji na hali zao.

Nchini Ugiriki, kupitia mpango wetu wa Maneno ya Usaidizi, tulifanya kazi na mashirika 20+, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 200+ na watu wa kujitolea kuhusu mawasiliano ya kitamaduni. Tulitafsiri maneno 800,000+ katika angalau lugha nane ili kukidhi mahitaji ya taarifa ya wakimbizi wengi iwezekanavyo.

Nchini Bangladesh na Myanmar, tumekuwa tukifanya kazi na mashirika yanayosaidia watu wa Rohingya tangu 2017. Tunaendelea kutoa usaidizi wa lugha na utafiti ili kufahamisha vyema mwitikio wa kibinadamu na kuboresha mawasiliano ya njia mbili.

Huko Ukrainia, tulikusanya rasilimali zetu kwa haraka kusaidia watu waliolazimishwa kuikimbia nchi. Tulifanya kazi na mashirika 49 ya ndani na kimataifa, katika miradi 276 ya kukabiliana na dharura iliyosababisha maneno milioni 1.5 kutafsiriwa katika lugha 35.

Katika Amerika ya Kusini, tulishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Ecuador, Meksiko na Peru kuunda Planeta Azul, chatbot ya usaidizi wa mtandaoni. Robotisogoa ilisaidia watu kupata huduma muhimu na taarifa katika mpaka wa Marekani na Mexico.

CLEAR Global inahitaji msaada wako katika

kuwapa wakimbizi na wahamiaji taarifa zaidi za kuokoa maisha.