Mazungumzo ya bilioni nne kuhusu
afya ya umma
Hapa CLEAR Global, tunasaidia watu kupata taarifa ya afya iliyo sahihi na yenye kuaminika, haijalishi wana zungumza lugha gani.
Tatizo: taarifa ya uwongo na taarifa iliyopotoshwa hutishia afya ya umma
- Taarifa ya uwongo na taarifa iliyopotoshwa hufanya milipuko ya magionjwa kuwa mibaya zaidi, kufanya milipuko hiyo kuwa migumu kushughulikia na kudhibiti.
- Kukosa imani kunakosababishwa na tetesi huwazuia wengi kuweza kupata tiba ya kitaalamu. Hilo lilitokea wakati wa wasiwasi wa kupokea chanjo ya COVID-19 katika nchi 15 za Afrika, Marekani, Ulaya, na milipuko ya Ebola katika Afrika ya Kaskazini.
- Vikwazo vya lugha vinaweza kuwa sababu kuu ya kusababisha taarifa ya uwongo. Uelewa wa taarifa ya afya hupungua kwa asilimia 78 wakati taarifa hiyo isipotolewa katika lugha mama ya mtu.
“Walitusaidia kuelewa changamoto ambazo watu wanakumbana nazo, ikiwa ni pamoja na taarifa za kina kuhusu hali za kuishi na hatari za afya. Wakati huo huo, inatusaidia kuadapt huduma zetu kwa utamaduni wa ndani, na hilo linalojumuisha kutoa katika lugha ya hapa."
Suluhisho ya CLEAR Global
CLEAR Global hutoa taarifa inayookoa maisha wakati wa majanga ya kiafya ili kusaidia kudhibiti milipuko ya ugonjwa na kutoa taarifa iliyothibitishwa.
Tunafanya tafiti ili kuelewa mahitaji ya watu ya habari na mawasiliano. Kisha tunaunda chaneli za mawasiliano zinazowawezesha watu kupata na kushiriki habari katika lugha yao. Pia, tunashirikiana na wakabilianaji waliothibitishwa na wanaoaminika ili kusambaza habari ya afya katika iliyofanyiwa majaribio katika miundo ya lugha nyingi.
Nchini Kenya, tulitambua mapengo ya mawasiliano yanayoathiri ukabilianaji wa Ebola. Mtu 1 kati ya 5 walielewa Kiingereza vizuri – watu walihitaji taarifa kwa Kiswahili. Hii ilisaidia kuweka kipaumbela tafsiri kwa Kiswahili ili kuhakikisha taarifa kupata taarifa inavyofaa na kupambana na taarifa potofu nchi nzima.
Nchini Nigeria, tuliunda Shehu, robotisogoa ya lugha nyingi iliyoundwa ili kuwasilisha taarifa zilizothibitishwa za COVID-19 na Ebola katika lugha ya Kihausa, Kikanuri, na Kiingereza. Ndani ya miezi sita ya uzinduzi wake, Shehu imetumika kwa ujumbe mfupi zaidi ya 80,000 ikiwa na watumiaji zaidi ya 5,750, wakipata asilimia 90.1 ya kiwango cha imani.
Nchini Bangladesh, tuliunda miongozo ya lugha ya Rohingya, ili wafanyakazi wa msaada wa huduma ya afya waweze kuwasiliana vema na watu. Rasilimali zetu husaidia kueneza taarifa sahihi na kupata imani ya watu katika mfumo, ili wajisikie huru kutafuta msaada wa afya na tiba.
CLEAR Global inahitaji msaada wako katika
kuandaa na kukabiliana na changamoto za afya za ulimwengu.