Mwenendo mbaya na udanganyifu

Kwa kuzingatia maono na maadili yetu, CLEAR Global imejitolea kudumisha kiwango cha juu cha maadili kati ya wafanyakazi wote, na inatarajia washiriki wote wa timu kutenda kwa njia inayolingana na maadili ya msingi ya ubora, uadilifu, uwezeshaji na uvumilivu wakati wa kutekeleza majukumu yao ya shirika. Wafanyakazi wote, wakufunzi, wanaojitolea na washauri wako chini ya kanuni za maadili. Mashirika tunayoshirikiana nao pia yanatarajiwa kutii viwango vya tabia vilivyoelezwa katika kanuni hii na kufuata viwango na kanuni za kisheria za kimataifa.

CLEAR Global inachukua uwajibikaji kwa uzito. Ikiwa una wasiwasi kuhusu mwenendo wa mfanyakazi yeyote wa CLEAR Global unaweza kutoa ripoti:

Katika kutoa ripoti hiyo, ingesaidia kujumuisha habari nyingi iwezekanavyo, kama vile tarehe na saa ya tukio, aina ya malalamishi, nani alihusika, walikuwepo mashahidi, jinsi matukio yalivyotokea, kama kuna wasiwasi juu ya usalama wa mtu, haswa, mtoto na kama huluki nyingine imepokea malalamiko haya pia.