CLEAR Tech itabadilisha pakubwa mawasiliano ya lugha nyingi.

Mawasiliano na upatikanaji wa habari hautoshani. Habari haipatikani katika lugha nyingi zilizotengwa.
Hizi ni lugha za watu wenye nguvu kidogo sana, hela au ushawishi katika jukwaa la dunia. Kwa maneno mengine, watu ambao wanahitaji habari zaidi hawawezi kuipata. Kwa msaada wako, tunaunda teknolojia ya lugha ya ubunifu na inayoweza kubadilika, kwa hivyo kila mtu ana sauti.

“Mawasiliano ni hitaji la msingi ambalo linaweza kusaidia kuokoa na kulinda maisha.”

Tatizo la pengo la lugha

Tulikuwa tunazungumzia mgawanyiko wa kidijitali. Lakini sasa tunaona mgawanyiko wa lugha – pengo kati ya watu wanaozungumza lugha zenye nguvu za kibiashara na za kimataifa na wale wanaozungumza lugha zenye nguvu kidogo. Pengo hili linazidi kuongezeka kila siku.

Watu wanaozungumza lugha za nguvu hawatatiziki kupata habari katika lugha yao. Na teknolojia imara ya lugha inawezesha habari mpya kutafsiriwa kwa ufanisi na mara nyingi.
Lakini kwa watu ambao hawazungumzi lugha za nguvu, habari wanayohitaji mara nyingi haipatikani. Teknolojia ya lugha ya kuunda habari mpya haipo. Tofauti hii inasababisha pengo la habari ambalo linapanuka kwa kasi.
Mahitaji ni ya dharura, na tunahitaji msaada wako.

Suluhisho la teknolojia ya lugha

Tuna uzoefu wa miaka mingi kuunda teknolojia ya lugha kwa lugha zilizo na rasilimali chache za teknolojia. Tumeunda robotisogoa za lugha nyingi kwa watu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria, Kenya, na Amerika ya Kati kupata habari za COVID-19, biashara endelevu, kilimo, na za huduma za wahamiaji na wakimbizi. Tuliteunda rasilimali za kutafsiri kwa lugha karibu 100, na tukajenga injini ya mashine ya kutafsiri kwa Kiarabu cha
Levantine kushughulikia ukosefu wa chakula.

Tuna mpango wa kushirikiana na watu bilioni nne ambao hawazungumzi lugha za nguvu, katika lugha wanayoelewa. Tunashirikiana na mashirika ya teknolojia ya ndani ili kuendeleza suluhisho zinazoweza kubadilika ambazo zinafaa watu, mahali, na shida. Tunafanya kazi na viongozi wa teknolojia ya kimataifa ili kuendeleza suluhisho rahisi, nzuri, zinazoweza kuzuilika. Na tunatafuta msaada wako ili kuunda suluhisho za mawasiliano ya usawa kupitia udhamini, maendeleo ya teknolojia, na mawazo mapya.

Unaweza kusaidia.

Maendeleo ya teknolojia ya lugha ni kipengele muhimu lakini mara nyingi hupuuzwa cha kujenga uhusiano zaidi na
ulimwengu wa usawa. Msaada wako unaweza kuwa na athari kubwa, kufikia watu zaidi, katika maeneo zaidi, na
lugha zaidi.
Kuwa sehemu ya suluhisho la mawasiliano ya kimataifa kwa kuwasiliana nasi hapa chini. Tutawasiliana hivi karibuni.