Taarifa za Fedha

Uwazi wa shughuli zetu ni kanuni inayoongoza hapa CLEAR Global. Tunafuata mwongozo kutoka kwa wasimamizi wa uwajibikaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali, ikijumuisha GuideStar na Foundation Center, ambao unapendekeza mashirika yote yasiyo ya kiserikali yadumishe uwazi katika kushiriki fedha, kama vile Fomu 990.

Taarifa maalumu kuhusu fedha za CLEAR Global inapatikana katika Fomu yetu ya 990, taarifa ya msamaha wa kodi ambayo mashirika huwasilisha kila mwaka kwa Huduma ya Mapato ya Ndani ya Marekani.

Tafadhali zingatia kwamba Fomu ya 990 imeandikwa kulingana na tarehe ya kuanza mwaka wa fedha, lakini ina taarifa hadi 31 Machi ya mwaka unaofuata. Hiki ni kipindi sawa na cha mwaka wa fedha wa CLEAR Global, ambacho kimeelezwa kulingana na tarehe ya mwisho ya mwaka wa fedha.

Vilevile, tulisajiliwa rasmi kama Translators without Borders kabla ya mnamo 2021.