
Translators without Borders (TWB) ni jamii ya kimataifa ya wanaisimu wanaosaidia watu kupata habari muhimu na kusikilizwa, haijalishi wana zungumza lugha gani.
Watu wanaozungumza lugha zilizotengwa mara nyingi hukosa habari muhimu katika lugha yao. Jamii yetu ya wanaisimu zaidi ya watu 100,000 hutoa muda na ujuzi wao kutafsiri habari muhimu kwa mamilioni ya watu duniani kote, ili kila mtu awe na habari anayohitaji na anayotaka.


"Inashangaza na pia inafariji sana na inatia moyo kuona watu wakitoa muda na ujuzi wao kutetea haki kanuni za utendaji pamoja na mawazo ya usaidizi wa kibinadamu.”
Field Manager for Doctors without Borders
Ukosefu wa habari iliyotafsiriwa
Wazungumzaji wa lugha zilizotengwa mara nyingi hawawezi kufikia maelezo wanayohitaji, kutaka na katika lugha na umbizo wanaloelewa. Hii inawazuia kupata taarifa kuhusu afya, kujifunza au haki zao.
Mashirika Yasiyo ya Faida na mashirika mengine ya kimataifa yanaweza kukosa utaalamu au ufadhili wa kuwasiliana na watu
wanaozungumza lugha hizi. Wanaweza kutatizika kupata wafasiri wanaofanya kazi katika lugha hizi au kujaribu kutegemea wafanyakazi wa eneo hilo kutafsiri, na hivyo kusababisha habari zisizoaminika, na hata kufanya wafanyakazi uwa na kazi kupita kiasi.
Kuna haja ya kulinganisha mashirika ya kibinadamu na yasiyo ya faida yenye wafasiri wenye utaalamu kote ulimwenguni. Hapo ndipo Translators without Borders huingia.

