
CLEAR Tech itabadilisha pakubwa mawasiliano ya lugha nyingi.
Mawasiliano na upatikanaji wa habari hautoshani. Habari haipatikani katika lugha nyingi zilizotengwa.
Hizi ni lugha za watu wenye nguvu kidogo sana, hela au ushawishi katika jukwaa la dunia. Kwa maneno mengine, watu ambao wanahitaji habari zaidi hawawezi kuipata. Kwa msaada wako, tunaunda teknolojia ya lugha ya ubunifu na inayoweza kubadilika, kwa hivyo kila mtu ana sauti.

“Mawasiliano ni hitaji la msingi ambalo linaweza kusaidia kuokoa na kulinda maisha.”
Editor, TC World
Tatizo la pengo la lugha
Tulikuwa tunazungumzia mgawanyiko wa kidijitali. Lakini sasa tunaona mgawanyiko wa lugha – pengo kati ya watu wanaozungumza lugha zenye nguvu za kibiashara na za kimataifa na wale wanaozungumza lugha zenye nguvu kidogo. Pengo hili linazidi kuongezeka kila siku.
Watu wanaozungumza lugha za nguvu hawatatiziki kupata habari katika lugha yao. Na teknolojia imara ya lugha inawezesha habari mpya kutafsiriwa kwa ufanisi na mara nyingi.
Lakini kwa watu ambao hawazungumzi lugha za nguvu, habari wanayohitaji mara nyingi haipatikani. Teknolojia ya lugha ya kuunda habari mpya haipo. Tofauti hii inasababisha pengo la habari ambalo linapanuka kwa kasi.
Mahitaji ni ya dharura, na tunahitaji msaada wako.



