CLEAR Global inawapa washirika huduma za lugha katika lugha anuwai kupitia Jamii ya TWB, mtandao wa kimataifa wenye wingi wa wanaisimu wanaojitolea zaidi ya 100,000. Wote hawa wanashiriki lengo la pamoja la kuongeza ufikiaji wa ufahamu kupitia lugha na kuhakikisha sauti za watu walio hatarini zaidi ulimwenguni zinasikika.
Uwezo wa Lugha wa Jamii ya TWB
Orodha hii ya Uwezo wa Lugha wa Jamii ya TWB inasaidia washirika wetu kuelewa ni rasilimali gani tuko nazo kwa sasa za huduma katika lugha tofauti.
Gundua chati ya Uwezo wa Lugha wa Jamii ya TWB– pata makadirio ya muda wa kukamilika kwa miradi katika lugha tofauti, kulingana na uwezo wa jamii yetu.
Wanajamii wote wa TWB wanashiriki imani na maadili yetu ya kimsingi na wanakubali kufuata Kanuni yetu ya Maadili kwa watafsiri.
CLEAR Global imeweka michakato ya uhakikisho wa ubora ili kuhakikisha kuwa timu za watafsiri zinafanya kazi katika kila mradi, ikiwezekana kukiwa na mkaguzi mwenye uzoefu zaidi anayekagua kazi ya wanajamii wengine.
Muda wa kukamilika kwa miradi ya huduma za lugha
Ingawa washirika wa CLEAR Global wanaweza kuomba huduma za lugha katika jozi yoyote ya lugha, tuna mwongozo ambao unapaswa kufahamu. Ifuatayo ni sampuli ya orodha ya lugha ambazo tuna uwezo mkubwa zaidi katika jamii yetu iliyopo ya watu wanaojitolea.
Iwapo lugha imejumuishwa katika orodha iliyo hapa chini katika kitengo cha Muda wa Kawaida wa Kukamilika, hii inamaanisha kuwa tunafanya kazi mara kwa mara katika lugha hiyo na kwa ujumla tunaweza kutoa tafsiri na masahihisho bila rasilimali zaidi, kulingana na Miongozo yetu ya Matumizi Yanayofaa.
CLEAR Global pia hutoa huduma katika lugha zilizo na idadi ndogo ya watafsiri wa kujitolea wanaopatikana, ambazo zinahitaji muda mrefu zaidi kukamilika. Tafadhali ruhusu muda zaidi wa kutafuta wakati wa kuomba huduma katika lugha hizi. Iwapo CLEAR Global haiwezi kutoa huduma katika lugha mahususi, tutakujulisha kwa wakati unaofaa.
Lugha zaidi na huduma zaidi za lugha
Wasiliana nasi ili kujadili mkakati wako wa lugha
- ikiwa unatafuta lugha zingine na lahaja za eneo husika ambazo hazijaorodheshwa hapa,
- au kujadili huduma za lugha isipokuwa kutafsiri na kukagua (maelezo ya sauti, manukuu, kudurufu, uhariri wa lugha rahisi, ujanibishaji wa programu/tovuti, unukuzi, uchapishaji wa eneo-kazi, uundaji wa istilahi lengwa, kukusanya na kuthibitisha data, nk.)
Kukuza uwezo wa lugha
CLEAR Global itajitahidi kutoa huduma ya miradi katika jozi yoyote ya lugha ili kukidhi mahitaji ya mashirika tunayoshirikiana nayo, kulingana na rasilimali zinazohitajika.
Tunapofanya kazi na lugha ambazo tunahitaji kutambua rasilimali zinazotegemeka na kukuza jamii yenye nguvu zaidi, CLEAR Global imeunda rasilimali za mafunzo. Hili inawezesha watu wanaojitolea katika lugha mpya kukuza ujuzi wao na sisi, hivyo kuruhusu washirika kunufaika kutokana na utaalamu wao wa lugha huku pia wakipata ujuzi wa kazi ya baadaye.
Mara kwa mara, tunafanya kazi na mashirika washirika ili kuajiri wafanyakazi wapya wa kujitolea katika Jamii ya TWB kwa lugha zilizotengwa na zenye rasilimali ya chini, na kukuza ujuzi wao.