Translators without Borders (TWB) ni jamii ya kimataifa ya wanaisimu wanaosaidia watu kupata habari muhimu na kusikilizwa, haijalishi wana zungumza lugha gani.

Watu wanaozungumza lugha zilizotengwa mara nyingi hukosa habari muhimu katika lugha yao. Jamii yetu ya wanaisimu zaidi ya watu 100,000 hutoa muda na ujuzi wao kutafsiri habari muhimu kwa mamilioni ya watu duniani kote, ili kila mtu awe na habari anayohitaji na anayotaka.

"Inashangaza na pia inafariji sana na inatia moyo kuona watu wakitoa muda na ujuzi wao kutetea haki kanuni za utendaji pamoja na mawazo ya usaidizi wa kibinadamu.”

Ukosefu wa habari iliyotafsiriwa

Wazungumzaji wa lugha zilizotengwa mara nyingi hawawezi kufikia maelezo wanayohitaji, kutaka na katika lugha na umbizo wanaloelewa. Hii inawazuia kupata taarifa kuhusu afya, kujifunza au haki zao.

Mashirika Yasiyo ya Faida na mashirika mengine ya kimataifa yanaweza kukosa utaalamu au ufadhili wa kuwasiliana na watu
wanaozungumza lugha hizi. Wanaweza kutatizika kupata wafasiri wanaofanya kazi katika lugha hizi au kujaribu kutegemea wafanyakazi wa eneo hilo kutafsiri, na hivyo kusababisha habari zisizoaminika, na hata kufanya wafanyakazi uwa na kazi kupita kiasi.
Kuna haja ya kulinganisha mashirika ya kibinadamu na yasiyo ya faida yenye wafasiri wenye utaalamu kote ulimwenguni. Hapo ndipo Translators without Borders huingia.

Jamii ya kimataifa ya wanaisimu

Jamii yetu ya wanaisimu hutoa zaidi ya maneno milioni 20 kwa mwaka. Wanatafsiri habari kwa ajili ya mashirika kote ulimwenguni, wakifanya kazi katika lugha zaidi ya 200 – kutoka Kiamhari hadi Kizulu.

Tunapanga kuendelea kukua na kusaidia jamii yetu ya wanaisimu. Tunaunda jamii za wafasiri katika lugha muhimu, kusaidia wanaisimu wapya katika ukuaji wao wa kitaaluma na mtandao. Tunaboresha teknolojia yetu ya lugha, kuboresha mfumo wetu na kujumuisha teknolojia mpya ya lugha ili kuipa jumuiya yetu zana inayohitajika ili kufanikiwa. Na tunaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya faida duniani kote ili kuunganisha wanaisimu na ujuzi wao na watu wanaohitaji taarifa.

Unaweza kusaidia

Unaweza kusaidia Jamii yetu ya Translators without Borders kupitia mchango, ufadhili au kwa kutumia ujuzi wako kama mwanaisimu.
Kuwa sehemu ya jamii ya kimataifa kwa kutembelea tovuti ya TWB.