Watu wanaozungumza lugha zilizotengwa wanahitaji msaada wako kwa dharura.

Watu bilioni nne kwa sasa wametengwa katika mazungumzo muhimu. Changia kusaidia kujenga ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kupata habari muhimu na kusikilizwa, bila kujali lugha wanayoizungumza.

idadi ya maneno yaliyotafsiriwa na wanalugha wetu kusaidia watu kupata habari za kuokoa maisha
0 + milioni.
lugha zilizotengwa ili watu waliotengwa zaidi waweze kupata rasilimali na huduma muhimu
0
wabia tulioshirikiana nao kutoa habari za lugha mbalimbali na kuunda teknolojia ya lugha
0
watu waliowezeshwa kushiriki katika mazungumzo muhimu katika lugha yao
0 + milioni.

Mabilioni ya watu wanashiriki mazungumzo mtandaoni kila siku. Tunategemea mtandao ili kujibu maswali muhimu na kushiriki katika mazungumzo ya dharura katika lugha za kawaida za mtandao kama Kiingereza, Kichina, na Kihispania.

Hata hivyo, zaidi ya watu bilioni nne bado hawawezi kupata haki msingi ya kibinadamu kupata na kushiriki habari za kuaminika.kwa sababu ni kidogo au hakuna kitu kinachopatikana katika lugha yao. Mchango wako unatusaidia kuunda rasilimali za lugha na zana za kuwasaidia watu ambao wamekimbia makazi yao, ambao wanakabiliwa na shida au maafa ya asili, kupata habari za kuokoa maisha na kusikilizwa.

Kwa kusaidiwa na jamii ya wanalugha ya Translators without Borders, CLEAR Global inaendeleza mazungumzo ya kimataifa, na kusikiliza watu, kwa lugha yoyote wanayozungumza.

Translators Without Borders translator talking in front of several seated men

Timu ya CLEAR Global inatumia uzoefu wa miongo kadhaa ya wa msaada wa kibinadamu wa kimataifa ili kuweka kipaumbele kwenye lugha na tafsiri katika majanga ya kibinadamu duniani kote. Tunatumia uwezo wa teknolojia ya lugha, na kuunda suluhisho kusaidia kuziba tofauti za kilugha kwenye mtandao. Tunaendeleza robotisogoa za lugha nyingi, vioski vya habari vinavyowezeshwa na sauti, ramani za lugha, na zana zingine za msingi za data ili kuendesha mabadiliko ya kimataifa katika mawasiliano, kuweka mahitaji ya watu kwanza.

Katika mwaka wa 2022 pekee:

  • Tulishirikiana na mashirika zaidi ya 45 ili kusaidia watu walioathirika na vita nchini Ukraine kupata habari muhimu katika lugha zao,
  • Tulianzisha upya Shehu, robotisogoa kuwawezesha watu kaskazini mashariki mwa Nigeria kupata majibu ya maswali yao ya COVID-19 kwa Hausa na Kanuri
  • Na tuliunda kioski cha habari ya Akili bandia (AI) ili kuwasaidia watu kujifunza kuhusu kilimo endelevu huko Bihar, India.

Saidia kukuza harakati zetu za Mazungumzo ya watu bilioni nne

Kuwa mtetezi wa kufanya sauti zilizotengwa zaidi zisikike. Tunataka kujumuisha watu bilioni nne katika mazungumzo muhimu ya kimataifa ambayo yanawaathiri.

Changia kwa CLEAR Global leo (USD).

Msaada wako ni muhimu. Saidia kuunda suluhisho za mawasiliano ambazo hufanya kazi kwa kila mtu, kwa lugha yoyote wanayoizungumza.

Jifunze zaidi na ueneze habari: Mazungumzo ya watu bilioni nne (#4 BillionConversations /#4BC)

Facebook
Twitter
LinkedIn

Tumekua kuzidi jina letu.

CLEAR Global ilikuwa ikiitwa Translators without Borders. Tumekua haraka zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita, na jina hilo haliashirii yote tunayoyafanya—lakini bado lipo kama kitengo chetu kikibwa na msingi wa operesheni yetu. Tembelea tovuti ya TWB hapa.